HERI YA MWAKA MPYA 2016
MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU, MIPAKA YA NCHI NA WATU WAKE
TUNAITAKIA TANZANIA YETU AMANI
MAISHA YETU BLOG
Jumamosi, 2 Januari 2016
Alhamisi, 31 Desemba 2015
Nakala Ulemavu
Na Lucy Ngowi
ELIMU ya mahitaji maalumu hutolewa kwa watoto wenye matatizo
ya kujifunza ili kuwawezesha kupata huduma za elimu.
Watoto hao ni wale walio na ulemavu wa kutokuona, viziwi,
ulemavu wa akili, ulemavu wa usonji, viziwi wasioona, ulemavu wa viungo na
walemavu wa ngozi.
Wenye mahitaji haya hutakiwa kupewa upendo wa hali ya juu
kutoka kwa wazazi, familia, walezi, jamii inayowazunguka na wanafunzi wenzao
shuleni ili nao wajione kuwa wanastahili kuwepo duniani.
Lakini kinyume cha hapo, huwaongezea maumivu na mateso watoto
hao, kwani kwa kutokuwapa elimu stahiki hilo ni tatizo ama kwa kutokupewa
huduma bora za chakula, malazi na mavazi.
Jamii inapotoa mapenzi ya kweli kwa watoto hawa hujisikia
furaha sana. Sasa basi ni vema jamii kuzidisha mapenzi ya dhati kwa watoto hawa
pamoja na serikali.
Mchango wa serikali nao unahitajika kwa kiasi kikubwa ili
kuwafanya watoto hawa wasiwe wapweke. Inatakiwa serikali itoe huduma zote
stahiki kwa watoto hawa ili waweze kusoma kwa bidii na hatimaye watakapomaliza
wapate nafasi nzuri kikazi.
Kwa upande wake Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
inajitahidi kuwa na shule pamoja na vitengo mbalimbali kwa ajili ya watoto hao
wenye mahitaji maalum, lakini zimekuwa
zikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za fedha na vifaa maalum kwa
ajili ya kufundishia.
Nimeanza kueleza hayo baada ya kupata nafasi ya kutembelea
Shule ya Msingi ya Katesh A, iliyopo wilaya ya Hanang mkoa wa Manyara.
Shule hiyo pia ni ya bweni kwa ajili ya kuwasaidia watoto
wanaoishi katika mazingira magumu ikiwemo wale wenye mahitaji maalum.
Katika shule hiyo ya Katesh A pia ni ya mchanganyiko kwa maana
kwamba inachukua watoto wenye mahitaji maalum, mazingira magumu na watoto wa
kawaida.
Wenye mahitaji maalum ni kama hao niliowaeleza hapo juu na
waliotoka kwenye mazingira magumu ambayo wazazi wao wamekuwa wakihama hama na
mifugo, kutokuelewana na maisha duni ya familia husika wapo 106.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Petro Tahhan anasema viziwi shuleni
hapo wanasoma madarasa tofauti, wasioona wanachanganywa darasa la tatu na wale wengine wasio na matatizo na wale wa
mtindio wa ubongo hufundishwa na walimu maalum.
Anaelezea changamoto za wasioona kuwa wana upungufu wa vifaa
vya kufundishia kama mashine za Braille. Mashine hizo zipo chache kwani
ilitakiwa kila mwanafunzi asiyeona awe na yake.
Tahhan anasema wanafunzi hao wasioona wapo nane, wavulana watano na wasichana watatu.
Darasa la awali yupo mmoja, la kwanza yupo mmoja, la pili wapo
wawili, la tatu wapo wawili na la tano wapo wawili.
“Mashine nzima ni mbili walimu ambazo walimu wanatumia lakini
kiuhalisia ilipaswa kila mwanafunzi awe na ya kwake. Kunatakiwa kuwe na walimu
15. Katika shule hii pia tuna walimu wasioona wawili ambao wanafundisha
madarasa ya kawaida,” anasema mwalimu huyo.
Anasema wanafunzi hao wasioona hawana vitabu vya kuwafundishia
kwa maana kuwa hawana vitabu vyao vinavyowahusu bali wanatumia vya kawaida.
Anasema miundombinu shuleni hapo sio rafiki kwani wanatakiwa
kuwa na mazingira rafiki na vyoo vyao wenyewe.
Pia wana upungufu wa vifaa vya michezo, hata viwanja vyao vya
kuchezea hakuna.
changamoto nyingine kwao ni suala la maji shuleni hapo ni
tatizo, hivyo inabidi wazoee mazingira hayo, mara nyingine wanachota wenyewe
ama wenzao wanawasaidia.
Na pia ulinzi ni shida shuleni hapo hakuna uzio.
Akizungumzia wanafunzi viziwi shuleni hapo anasema wapo 27 ambao wanatakiwa kusoma miaka
10 badala ya saba ya kawaida. Darasa la kwanza, la tatu na la tano wanasoma
miaka miwili miwili.
Wanasoma kwa mfumo huo kwa kuwa wanakuwa wanachelewa kuelewa
kile mwalimu anachofundisha, ila madarasa mengine wanasoma mwaka mmoja mmoja.
Anasema shule hiyo ina upungufu wa vyumba vya madarasa hivyo
wakati mwingine wanachanganywa wote katika chumba kimoja, pia wana tatizo la
walimu wenye uwezo wa kufundisha watoto hao wenye mahitaji maalum.
Jambo lingine ni kwamba mihtasari wanayotumia ni ya kawaida
haiendani na mahitaji yao.
Tatizo lingine ni kwamba hawana kamusi yao ya lugha ya alama.
Analitaja kundi lingine ni la albino ambao hivi sasa wapo
nane, awali walikuwa 11 lakini watatu wamemaliza. Wanafunzi hao wanakabiliwa na
tatizo la vifaa vya kujikingia ngozi yao kama mafuta yao na kofia.
Mwalimu mkuu huyo anasema wale wa utindio wa ubongo wapo
watano, kati ya hao wawili ni wa kiume na watatu wasichana.
“Hawa wa utindio wa ubongo kwa sasa wapo nje ya shule. Wana
upungufu wa walimu, mihtasari yao hakuna, hivyo kwa sasa wanapelekwa na wazazi
wao shuleni hapo,” anasema mwalimu huyo na kuongeza kuwa kitengo hicho cha
utindio wa ubongo kimeanza mwaka huu.
Kwa wanafunzi hao wa utindio wa ubongo, wanafundishwa na
mwalimu wa kiume lakini walitakiwa walimu wa kike pia kwa sababu wanahitaji
huduma za ziada kama kusaidiwa kwenda chooni ama kulishwa ama wakati mwingine
kuvalishwa nguo kama wamejichafua.
Anasema kuwa shule hiyo haina mipaka wanaweza kwenda kutoka
mikoa yote nchini, kwani mbali na wakutoka wilaya hiyo wengine wanatoka Tanga,
Simanjiro, Singida, Babati na Mbulu.
Tahhan anashauri shule hiyo ingeangaliwa kwa jicho la kipekee
kwa kuwa ni shule ya mahitaji maalum, kwani fedha wanazopewa ni kwa ajili ya
chakula tu, hakuna ya kumlipa mlezi wala vinginevyo.
Kwa upande mwingine Mwalimu Mkuu msaidizi Caroline Lema
anasema kama serikali imeamua kutenga shule hiyo hapo Hanang iwasaidie watoto
kwa kuwapa vifaa vyao stahili ili ule umaalum uonekane.
“Watoto hawa inatakiwa watibiwe walau kwa mwaka mara mbili,
kama ni wasioona inabidi wachunguzwe wote uoni wao lakini kwa pesa inayotolewa
inatosheleza kwa chakula tu, sasa hii ni elimu maalum kwa vipi? kama hata hela
ya matibabu hakuna?,” anahoji Lema.
Mwalimu huyo anasema kuna watoto watatu ambao wanatakiwa
waende katika hospitali ya KCMC Kilimanjaro kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji
haraka iwezekanavyo lakini kwa kuwa hakuna fedha hawajaenda.
Anasema kila halmashauri yenye elimu maalum huwa anakuwepo
ofisa elimu maalum lakini anakuwa na fani moja labda ya viziwi sio utindio wa
ubongo, lakini anafikiri ilibidi kuwe na maofisa mchanganyiko ama huyo ofisa
asiwe amejikita kwenye eneo moja tu.
Kwa upande wake mwalimu Anna Mark anayefundisha wanafunzi
wasioona shuleni hapo anasema changamoto kubwa ni ukosefu wa vifaa vya
ufundishaji.
“Vifaa vingi tunaweza kuvitengeneza wenyewe ambavyo
vinawasaidia watoto hawa,” anasema mwalimu huyo na kuongeza kuwa upungufu wa
mashine za Braille ni changamoto kwake na wanafunzi hao.
Akiwaelezea watoto hao jinsi wanavyopokea kile
anachowafundisha anasema wanajitahidi kupokea vizuri japo kwa taratibu sana.
Mwanafunzi wa darasa la pili Imani Agustine anasema anapata
ugumu pale anapoandikiwa neno jipya hata kama amefundishwa anashindwa kulisoma.
Naye Paulo Marcelly anasema somo la hisabati linampa shida
hivyo anaiomba serikali kuwapatia vitabu na mashine.
Naye Ofisa Elimu Maalum wa Hanang, Albart Machua anasema
katika shule ya Katesh A kuna changamoto nyingi sana ikiwemo vyumba vya madarasa na vifaa vya kufundisha na
kujifunzia.
Anasema kuhusu fedha za matibabu za wanafunzi hao hutolewa na
halmashauri, japo kuna baadhi ya wanafunzi walihitajika kwenda KCMC kufanyiwa
upasuaji wa macho, hawakwenda kwa kukosa pesa.
Pia anaomba serikali ijitahidi kufikisha hela za ruzuku kwa
wakati ili wanafunzi hao waweze kuhudumiwa.
Kwa upande wake Ofisa elimu wa wilaya ya Hanang, upande wa
shule ya msingi, Gwandu Omari anasema wanafunzi hao wanatakiwa watengwe
kutokana na ulemavu walionao.
“Katika shule ya Katesh A kuna changamoto ya mabweni yaliyopo
hayatoshi, ni chakavu, magodoro machache, jiko na bwalo vyote vina upungufu,”
anasema.
Pia anasema baadhi ya fani zinazohusu watoto wenye mahitaji
hayo kuna upungufu wa walimu, wapo watano ila mahitaji ni 13.
Hata mashine za watoto wenye shida ya macho ni chakavu
zinafanyiwa matengenezo kila wakati, karatasi zake ni za shida.
Viziwi wanatakiwa wawe na mashine na tochi za kuwakagua hali
zao za masiko kila wakati lakini hakuna.
Albino nao ni shida huduma zao, wanahitaji kuchekiwa ngozi zao
mara kwa mara. Kuna gharama za kila wakati kliniki na kupewa mafuta maalum.
“Hawa wa mtindio wa ubongo huduma zao ni za karibu sana popote
anahitaji msaidizi, inapokuwa ni mwalimu peke yake kazi inakuwa kubwa,”
anasema.
Akizungumzia miundombinu bado kuna tatizo kubwa hakuna ufumbuzi wa haraka wa kuongeza
madarasa na mabweni yaliyopo ni chakavu yanatakiwa kubomolewa.
Kwa upande wake Mratibu wa Elimu Maalum kutoka wizara ya
elimu, Gryson Mlanga anataja idadi za shule maalum na vitengo katika maeneo
mbalimbali nchini.
Mlanga anasema idadi za shule kwa wasioona zipo nne Tanzania
nzima ambazo ni Irente Lushoto, Buigiri Chamwino, Malangali Sumbawanga na
Furaha Tabora.
“Hizi ni shule maalum. Uoni hafifu na albino na wasioona
kabisa,” anasema.
Kwa upande wa shule mchanganyiko zipo 34, ambapo katika shule
hizo darasa la kwanza na la pili wanakuwa na madarasa maalum, kuanzia la tatu
mpaka la saba wanachanganyika na wasiokuwa na ulemavu.
“Hizi shule zina mabweni. Nazo ni uhuru mchanganyiko iliyoko
Dar es Salaam, Pongwe Tanga, Same Kilimanjaro, Mwereni Moshi, Longido, Katesh A
wilayani Hanang, Ikungi Singida na Hombolo mkoani Dodoma,” anasema.
Mratibu huyo anasema
kwa viziwi shule maalum zipo 11 na vitengo 37. Vitengo ni vile vinakuwepo
kwenye shule za kawaida ambapo hutengwa madarasa maalum.
Anataja baadhi ya shule hizo za viziwi kuwa ni Buguruni,
Mwanga, Njombe, Tabora viziwi, Twivila Iringa na Tumaini Singida.
Baadhi ya vitengo kwa viziwi ni Mugeza huko Bukoba, Msasani
Dar es Salaam, Maweni Kigamboni, Twiga eneo la Temeke na Basil Mramba huko
Mwanga, Kilimanjaro.
Kwa upande wa ulemavu wa akili zipo shule tano maalum ambazo
ni Sinza maalum, Mtoni Maalum, Miyuji Dodoma, Bethlehemu Ifakara na Lulindi
huko Masasi.
Ina zaidi ya vitengo 250 ambavyo ni Leganga Arusha, Rutihinda
Kinondoni, Umoja Kinondoni na Msasani zote zikiwa mkoa wa Dar es Salam.
Ulemavu mwingine ni ule wa usonji ambapo watu hao wameathirika
katika mishipa ya fahamu, unaathiri mahusiano, ufahamu na mawasiliano.
Katika huo kuna vitengo vitano kwa Dar es Salaam na Morogoro.
Vipo Msimbazi Mseto, Patandi na Uhuru Arusha, Kiwanja cha ndege Morogoro na
Mbuyuni.
Wengine ni wanafunzi wasioona amboa wako kwenye vitengo. Uhuru
mchanganyiko, Mwanga, Mugeza Bukoba, Makalala Mufindi na Katumba Two, Tukuyu.
Akizungumzia wenye mahitaji maalum ya ulemavu wa viungo husoma
kwenye shule za kawaida kama hawana shida kubwa.
Hao wenye ulemavu wa viungo wengine huwepo Jesho la Wokovu
jijini Dar es Salaam, Faraja mkoani Kilimanjaro, Malangali, Kabanga Kasulu
mkoani Kigoma huko nako wapo wasioona na albino. Na Siuyu mkoani Singida.
Mratibu huyo anasema changamoto zipo na wanazipata kwenye
taarifa mbalimbali zinazowafikia, pia wanapopata fursa za kutembelea shule hizo
hukutana nazo.
Akielezea mahitaji wanayopaswa kupewa wanafunzi hawa kutoka
serikalini ni chakula, malazi safi, matibabu, nauli wakati wa likizo, vifaa vya
kufundishia na vya kujifunzia kulingana na mahitaji husika.
“Kama wizara tunatarajiwa watoto hawa wahudumiwe katika maeneo
hayo,” anasema.
Kuhusu vifaa vya watoto hao, anasema kwa muda mrefu
vilinunuliwa na wizara, lakini ikafika mahali ikaamuliwa vitolewe na
halmashauri na sasa hivi kuna mradi unaotekelezwa nchi nzima wa kuvinunua.
“Zitanunuliwa mashine 800 za Braille, shime sikio 1000, fimbo
nyeupe 1200 pia tunaendelea kuchapisha vitabu 8000 ambavyo vitasambazwa vya
mtaala mpya,” anasema na kuongeza kuwa vifaa hivyo vitatolewa kabla ya mwaka
huu haujaisha.
Anasema suala la walimu ni jukumu la Ofisi ya Waziri Mkuu –
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Anasema mpango wa baadaye ni kwamba kila halmashauri iwenna
shule moja maalum kwa ajili ya wanafunzi wa mahitaji maalum.
Anasema takwimu sahihi za wanafunzi hao hazipo ila kuanzia
sasa zinaanza kukusanywa mpaka mwaka 2020 zitakuwa zipo tayari.
mwisho
Ukatili wa Kijinsia Hanang
Daftari laandaliwa kudhibiti utelekezaji wa familia Hanang
- Linawabana wanaume kutoa matumizi kwa watoto kwa kusaini
Na Lucy Ngowi
UKATILI wa kijinsia maana yake ni unyanyasaji wa aina yoyote
anaokutana nao mwanaume au mwanamke kwa sababu tu ya jinsia yake.
Kwa mfano shambulio la mwili kama kumpiga mwanamke. Watu wengi
kutokana na mfumo dume ulioko wanadhani kuwa kitendo hicho ni sawa kumbe sio.
Katika wilaya ya Hanang una ukatili wa aina nyingi ukiwemo wa
kutelekeza mke, watoto ama vipigo kutokana na ulevi uliokithiri kwa wanaume.
Ofisa maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Hanang, Sabina Sulle
anasema ukatili mkubwa wa kijinsia upo
kwenye utelekezaji wa watoto.
Anasema katika wilaya ya Hanang kesi za kutelekeza watoto zipo
nyingi kwani wanaume wengi sana wanakwepa jukumu lao. Hivyo wanawake
wanapozidiwa ndipo utafuta msaada kwao.
Anasema wanakutana na changamoto sana katika kutatua kesi za
aina hiyo kwa kuwa wanaume wengi ni waongo, wanaahidi kuwahudumia baada ya
kufikishwa kwao lakini, hawatekelezi.
Kutokana na hali hiyo imewabidi wawe na daftari ofisini ambapo
mwanamme akikubali kuhudumia watoto wake kila mwisho wa mwezi anapeleka pesa
hapo na kusaini, na mwanamke anakwenda kuchukua hapo hapo ofisini na kusaini,
jambo ambalo limesaidia sana.
Anasema kesi kama hizo kwa mwaka huu zinazidi 30.
Kwa upande wake Mratibu wa Hanang Women Conceling and
Development Association Mary Gitagno wa kata ya Ganana, anazungumzia ukatili wa
aina nyingine ni kurithiwa baada ya mume kufariki.
“Ukatili mwingine ukifiwa unarithiwa. Kwanza unatakaswa.
Wakati unaendelea kupata maumivu ya mume wako aliyefariki, anakuja mnyaturu
analeweshwa pombe usiku, mwanamke unapewa sehemu ya kulala siku hiyo unajikuta
uko mwenyewe, mnyaturu huyo anakuja kufanya tendo la ndoa na analipwa ukikubali
unakuwa umeshatakaswa,” anasema Gitagno.
Anasema wanawake wengi hawapendi hali hiyo hukataa na
kukimbia, ndio chanzo cha kupoteza mali za mume wake.
Anasema mambo mengi ya mila kama hayo hufanywa kisirisiri bila
wengine kujua.
Mama mmoja Neema Alex (jina lisilo rasmi) mwenyeji wa Kata ya
Basuti, tarafa ya Basuti, anasema mume wake alipofariki miaka mitano iliyopita,
aliletewa mtu kwa ajili ya kutakaswa.
Kwa maelezo ya mama
huyo, siku hiyo jambo ambalo sio la kawaida alijikuta akiwa amelala mwenyewe
wanawake wenzake wakiwa hawako, usiku ulipokuwa mwingi, akaja mlevi mmoja na
kutaka kumwingilia kwa nguvu, alishtuka na kukimbia.
Mtu Yule aliyeandaliwa alienda kudai ujira wake kwa
waliomwagiza, huku nyuma yeye alikuwa akitafutwa ili apigwe lakini alikimbia na
kwenda polisi.
Anasema kama jambo hilo lingefanikiwa angerithiwa na ndugu wa
mume wake.
Anasema kwa kufanya hivyo ndio maana wanawake wengi wa
vijijini wanaambukizwa magonjwa mbalimbali.
Daktari wa Kituo cha Afya cha Katesh, David Laizer anasema
ndoa za utotoni zinazosababishwa na wazazi ni ukatili mkubwa, kwa kuwa kitendo
hicho si kwa ridhaa ya muolewaji.
Pia anasema ukatili mwingine anaouana ni ule wa kuwapeleka
watoto wa kiume shuleni na kuwaacha wa kike. Huo ni ukatili uliopitiliza kwa
jamii hiyo.
Pia wanaume kutelekeza wake zao na watoto ni ukatili mkubwa
kwa kuwa watoto wale wanateseka kwa kukosa mahitaji muhimu.
Wengi wanatelekezwa ama kuachika wanakuwa hawana sehemu za
kwenda hali inayoleta mateso kwa watoto.
Kwa upande wake Mtendaji wa Katesh, Peter Mando anasema katika
eneo hilo ukatili wa kijinsia upo sana kwa wanaume kuwapiga wake zao pamoja na
kuwafukuza nyumbani.
“Migogoro kama hii tunaisuluhisha sana sisi na maofisa wa
jamii, mahakama na polisi. Bado changamoto hiyo ni kubwa sana,” anasema.
Anasema katika kutatua migogoro hiyo wanawatumia maofisa wa
maendeleo ya jamii kusuluhisha ikiwa ni pamoja na wazee wa mila na mahakama.
Chanzo cha jambo hili anasema ni mila na desturi za huko kwani
wanaume wamekuwa wakiwabeza sana wanawake, ugumu wa maisha kwani wanandoa wengi
wamekuwa wakizozana kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani.
Si hivyo tu, bali na unywaji wa pombe pamoja na kutokufanya
kazi, ndiyo inaleta shida hii.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Katesh A, Petro Tehhan anasema
ukatili wa kijinsia eneo hilo unasababishwa
na mfumo dume pale baba anataka kusema kila kitu.
Pia kutokuelewana kwa mume na mke kunasababisha hali hiyo.
Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Hanang Kituo cha Katesh, Hamis
Mwampelwa anazungumzia kesi za ukatili wa kijinsia zilizoripotiwa kituoni hapo
ni 161, kati ya mwaka 2014 hadi sasa.
Anasema katika kesi hizo zile zilizofungwa ambazo
hazikufikishwa mahakamani ni kesi 38, zilizofikishwa mahakamani ni 59 na zilizo
chini ya upelelezi ni 70.
Kati ya kesi hizo, Mwampelwa anasema zilizopata mafanikio ni
15, ambazo hazikupata mafanikio ni 14, kesi iliyopo mahakamani kwa mwaka huu ni
moja.
Anaeleza miongoni mwa kesi zilizoripotiwa za unyanyasaji wa
kijinsia kuwa ni zile za kutelekeza familia, kubaka, shambulio la aibu pamoja
na ukatili dhidi ya mtoto.
Anatoa mfano kwa kesi moja iliyofikishwa kituoni hapo siku za
karibuni.
Kesi hiyo inamhusu mkazi wa Kitongoji cha Qedang’onyi Emanuel
Lambo (50), aliyetarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kumtendea vitendo vya
ukatili mtoto wake wa miaka tisa wa shule ya msingi kwa kumchoma na kisu chenye
moto mkali maeneo mbalimbali ya mwili.
Mwampelwa anasema mtoto huyo alichomwa moto maeneo mbalimbali
ya mwili, kwenye kiwiko mkono wa kulia,
kwenye shavu kushoto, shingoni kushoto, usoni na sehemu mbalimbali za mguu
upande wa kulia kutokana na kulala kwa kaka yake, Mussa Emmanuel.
Anasema Oktoba 15 sueta la shule la mtoto huyo lilikuwa
halijakauka, mama yake akamwagiza kaka yake akamuombee ruhusa shuleni, kisha
mtoto huyo akalala kwa kaka yake huyo ndio ilikuwa chanzo cha baba kutenda
ukatili huo.
Anasema mwanafunzi huyo aliwaambia wakati akitendewa ukatili
huo, mama yake alijitahidi kumwokoa lakini baba yake alimkataza.
Tukio hilo la mwanafunzi kutendewa ukatili, lilijulikana baada
ya mwalimu wake Bahati Mwiru kuhakiki wanafunzi shuleni na kugundua mtoto huyo
hayuko, ndipo wenzake wakamwambia ana majeraha.
“Mwalimu aliendelea kuuliza wanafunzi hao majeraha ni ya nini, ndipo wakamwabia amechomwa moto
na kisu. Wakaijulisha kamati ya shule, mwenyekiti na mlinzi wakaenda kumchukua
nyumbani,” anasema.
Anasema mwalimu huyo alitoa taarifa polisi baada ya mtoto huyo
kukosekana shuleni kwa muda na alipouliza wenzake walimwambia anatibu majeraha
aliyosababishwana baba yake, ndipo wakaanza kumfuatilia.
mwisho
Ukeketaji Mbulu
Helena Ringo: Mimi ni mfano wa watu waliokeketwa
Joan Michael: Nilipokeketwa damu na usaha ilitiriria
DK.Leonard Tlatlaa: Nimekutana na mtoto njia ya uzazi imefunga
kwa ajili ya kukeketwa
Na Lucy Ngowi
“NAKUMBUKA nilipokuwa na miaka mitano nilikeketwa. Kiukweli
sitaisahau siku hiyo kutokana na maumivu niliyoyapata wakati wa kukeketwa na
kuuguza kidonda.
“Wakati naugulia maumivu ya kukeketwa, nilikuwa nikiona katika
sehemu zangu za siri damu na usaha vikitiririka, ila sijui mbele ya safari
itakuwaje, kama atakuwa na uwezo wa kupata mtoto au la,” anasema Joan Michael
(jina lisilo rasmi).
Binti huyo ambaye hivi sasa ana miaka 19 anazungumza kwa
uchungu kuelezea mila potofu zinazofanywa na kabila lake la wabarbaig.
Anasema laiti kama angechelewa kukeketwa asingekubali tena
kwani katika hali ya uhalisia ni ukatili uliopitilizwa, kwani hata kwenye
maandiko matakatifu biblia hakuna mahali inapozungumzia kuhusu kumkeketa
mwanamke bali kutahiri wanaume.
Anaiomba Serikali kuendelea kutoa elimu bila kuchoka kwa jamii
hiyo ili kuwanusuru watoto wa kike ambao bado hawajakeketwa wasipatwe mateso
ambayo alikabiliana nayo.
Si huyo tu, mfano wa binti
kama huyo ni mingi katika jamii za watu wanaokeketa ila wamekuwa
wakiogopa kuzungumza hadharani kwa kuona aibu au kuhofia kutengwa na ndugu
zake.
Kwa upande wake Mama Mchungaji wa Kanisa la Evangelistic
Assemblies of God (EAGT), Odeliana Emmanuel anasema katika kijiji cha Qandach
alikozaliwa, kata ya Endamila wilaya ya Mbulu, amekuwa akiona hali ya ukeketaji
kwa watoto wa kike.
Anasema kama mama mchungaji na mwanaharakati wa kumtetea mtoto
wa kike, amekuwa akizungumza na wale wanaowaandaa watoto kuwapeleka kwa
ngariba, kuwaelimisha na kuwafundisha athari za kukeketwa kwa mtoto wa kike.
“Nimeelimisha ubaya wa ukeketaji. Kwa sasa umepungua lakini
unaendelea kwa siri sana, hivyo wamebadili mbinu mpya ya kuwakeketa watoto
kuanzia wanapoanza kutembea,” anasema mwanaharakati huyo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Mbulu, Halmashauri ya
Vijijini Justino Bayo anasema wilaya hiyo ina wenyeji wanaojulikana kama
wairaqw, datoga au barbaig, nyisanzo na hadzabe.
Anasema suala la ukeketaji katika wilaya hiyo sasa hivi
linapungua kwa wairaqw pamoja na wanyisanzo, lakini wa wabarbaig wanaendelea.
Lakini kama tendo hilo linafanyika katika mji huo ni
kwa siri sana kutokana na kuogopa mkono wa sheria.
Bayo anasema chanzo cha hilo ni mila na desturi za wenyeji
ambao wanaona kuwa mwanamke asipokeketwa ni kama najisi.
Naye Helena Ringo anaeleza kuwa, yuko miongoni mwa
waliokeketwa, kwani mbaya zaidi alifanyiwa kitendo hicho akiwa na miaka 19
baada ya kumaliza chuo.
“Mimi ni mfano wa watu waliokeketwa. Nilikeketwa nikiwa
nimemaliza chuo cha ualimu nikiwa na miaka 19,” anasema.
Mwanamke huyo ambaye fani yake ni mwalimu pia ni Mratibu wa
Shirika linaloshughulikia ukeketaji wanawake na wasichana (AFNET), anasema mara
nyingi mwisho wa mwaka wanawake wengi wanaandaa wasichana wao kwa ajili ya
kukeketwa.
Hivyo kama mwanaharakati amekukwa akipita shule mbalimbali na
kuwaasa wanafunzi wasikubali kukeketwa kipindi cha likizo.
Anasema amekuwa akipita katika shule za msingi na kutoa elimu
hiyo, si hivyo tu bali mara nyingi pale anapokuta watu wamekusanyika huomba
nafasi na kusema machache kuhusu ubaya wa ukeketaji.
“Nimekuwa nikiwaambia msipunguze kiungo chochote cha mtoto
katika mwili wake, endapo mtafanya hivyo akimkamata mtu yeyote anampeleka
mahakamani,” anasema mwanaharakati huyo.
Si hivyo tu, bali hata siku ya mtoto wa Afrika inayofanyika
Machi 16, huwa anatoa elimu hiyo kuhusu ukeketaji.
Anakiri kuwa tatizo hilo ni kubwa, hivyo kama wataendelea
kutoa elimu litapungua.
Anaongeza kuwa, baada ya kutolewa elimu mara kwa mara kuhusu
athari za ukeketaji tatizo linapungua isipokuwa kwa watu wa vijijini ambao
hufanya kimya kimya ili wasijulikane
wanachokifanya.
Ringo anasema chanzo cha ukeketaji ni imani iliyojengeka kuwa
wanawake wanakeketwa ili kupunguza uhuni, lakini kiuhalisia ndio waliozidi kwa
tabia hiyo mbaya.
Sababu nyingine ni kwamba wanamfanyia usafi msichana huyo kwa
sababu sehemu hiyo inaficha uchafu.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Mbulu, Dk.
Leonard Tlatlaa anasema hawajapata kesi za mtu aliyezidiwa kutokana na
kukeketwa lakini kama daktari anaona kuna dalili zinazoonyesha bado kuna
ukeketaji.
Na kwamba katika eneo hilo wanakeketa watoto katika umri mdogo
kwa kuogopa mkono wa sheria.
“Kama daktari nimekutana na kesi ya mama wa mtoto kusema mtoto
wake hana njia ya uzazi, nilipomcheki nikagundua njia iko wazi na kuna kidonda
kilichotokana na kukeketwa,” anasema.
Anaongeza kuwa kati ya mwaka jana na mwaka huu amekutana na
wagonjwa watatu wenye matatizo yaliyosababishwa na kukeketwa. Anasisitiza
ukeketaji uliopo hivi sasa unafanywa katika umri mdogo.
Akizungumzia athari za ukeketaji ni kupoteza damu nyingi, pale anapokeketwa mtu kinatokea kidonda na
kutengeneza usaha ambao hupandisha homa na kuleta ufinyu wa njia ya uzazi hivyo
mama wakati wa kujifungua huchanika.
Anasisitiza katika wilaya hiyo ukeketaji upo kila mahali.
Chanzo chake ni mila na desturi kwa kuwa watu hawataki
kubadilika , pia wanasema kama msichana hajakeketwa hafai kuolewa. Hiyo ni
dhama potofu.
Anasema pamoja na elimu inayotolewa jamii bado haijakubaliana
na hiyo dhana ya kutokukeketa kutokana na mila na desturi. Hiyo ni kasumba yao
bado haijawatoka.
Anashauri elimu iendelee kutolewa kuhusu athari zake baadaye
kuhusu uzazi bora.
Pia hata mkono wa sheria unapokuwepo ufuate mkondo wake.
Mratibu wa Shirika la Afya na Maendeleo (Gesodea) pia
Mwenyekiti wa Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya mtoto mdogo, Tawi la
Manyara Jackson Suloo anakiri ukeketaji
Mbulu umepungua kutokana na elimu inayoendelea kutolewa.
Pia anaamini miaka ijayo tatizo hilo litakuwa limekwisha, na
kwamba tokea mwaka jana hadi sasa taasisi yake imezungumza na wazazi 83 kuhusu
athari za ukeketaji.
Anaelezea chanzo cha ukeketaji ni kwamba ngariba wanatafuta
kipato.
Kwa upande wake WP 4728 Koplo Glory kutoka kituo cha Polisi
Mbulu anayeshughulikia dawati la jinsia anasema, kituoni hapo hakuna kesi
zozote za ukeketaji zilizofikishwa.
Wilaya ya Mbulu ni mojawapo ya wilaya zilizopo katika Mkoa wa
Manyara. Katika sensa ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa
kuwa 320,279 waishio humo.
Mbulu imepakana na Mkoa wa Arusha pamoja na ziwa Eyasi upande
wa kaskazini, wilaya ya Babati Vijijini upande wa mashariki, wilaya ya Hanang
upande wa kusini na mkoa wa Singida kwa magharibi.
Wenyeji asilia ni Wairaqw
ama wanajulikana kama Wambulu. Makao makuu yapo Mbulu mjini na mji huu
ulianzishwa wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa jina la
Neu-Trier.
Ukeketaji hapa nchini badi upo katika baadhi ya maeneo kama mkoa wa Manyara, Dodoma, Arusha,
Singida, Mara, Kilimanjaro na Morogoro.
Kati ya mikoa hiyo saba, Mkoa wa Manyara ndio unaongoza kwa
asilimia 70.8 na Morogoro ndio wa mwisho kwa asilimia 21.1.
Ndoa za utotoni
Na Lucy Ngowi
NDOA za utotoni huathiri afya kwa kuwa mwili wa mtoto unakuwa
hauko tayari kukabiliana hali hiyo, pia huleta athari za kisaikolojia.
Katika Wilaya ya Hanang, Mkoani Manyara kuna tatizo la kuwepo
kwa ndoa za utotoni hali inayosababisha wasichana kupata mimba katika umri
mdogo.
Inaelezwa kuwa katika wilaya hiyo ndoa za utotoni zipo lakini
sio kama ilivyokuwa zamani, na kwamba watoto wanavyoolewa sio hiari yao bali
hulazimishwa na wazazi wao.
Hapo zamani kwa kabila la wabarbaig msichana alikuwa
haruhusiwi kuzungumza lolote kuhusu kijana anayempenda, ila wazazi ndio
walikuwa wakiwatafutia wachumba.
Ama msichana anapokuwa akichunga kijana anayempenda humkamata
na kuishi naye, kwa siku chache endapo msichana atarudi nyumbani kwao, wazazi
wa binti huyo humrudisha kwa kijana huyo.
Mwanamke Anna Mussa (jina lisilo rasmi), anasema alipewa mimba
akiwa na miaka 12, hivi sasa ana watoto watano.
Anasema akiwa katika hali hiyo
mwanzoni haikuwa rahisi kwa kuwa hakuweza kumudu maisha ya ndoa, lakini
kwa kuwa mwanamme huyo aliamua kuishi naye hivi sasa wana watoto hao watano.
Kwa maelezo yake alizaliwa mwaka 1979, hivi sasa ana watoto
wakubwa kabisa ambao wengine wameolewa na kuoa na wengine bado wapo shuleni.
“Kwangu mimi niliona kama nimepata bahati kwa kuwa vijana
wengi wanawapa wasichana wadogo mimba kasha huwakimbia, hawako tayari
kuwahudumia kwa jambo lolote lile. Huyu wa kwangu alikubali tuendelee kuishi
hadi hivi leo,” anasema mwanamke huyo.
Akizungumzia hilo Ofisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Hanang,
Sabina Sulle anasema ndoa za utotoni zinaenda sambamba na mimba za utotoni.
Watoto wengi wanaopata mimba hufika ofisini kwao kwa ajili ya
kulalamikia kutopata matunzo ya watoto au mtoto aliyezaliwa.
Anasema kesi za utelekezaji wa watoto ofisini kwao zipo
nyingi, ambazo hupelekwa hapo kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa jinsi ya kumlea
mtoto au watoto waliozaliwa.
Anasema ofisini kwao, wana kesi ya binti moja mwenye miaka 17
ambaye alipata mimba utotoni.
“Binti huyo alizaa na mume wa mtu, hivyo akawa hapati matunzo
baada ya kujifungua. Kesi ilipofika kwetu tukaitatua kwa kumwamuru mwanamme
huyo kumtunza mtoto hadi atakapofikia miaka 18,” anasema.
Pia ushauri mwingine wanautoa wanashauri mtoto atakapofika
miaka 17 anatakiwa kuulizwa kama anataka kuishi na baba yake.
Anasema kesi nyingine walizonazo ni za kutekeleza watoto. Hizo
zipo nyingi kwa kuwa wanaume wengi hawawatunzi watoto hivyo pale wanawake
wanapozidiwa huenda ofisini kwao kutafuta msaada.
Pamoja na kutatua kesi nyingi, ofisa huyo anasema kuna
changamoto zake kwani wanaume wengi ni waongo wanaweza kuzungumza kuwa
watawatunza watoto baada ya kufikishwa hapo lakini utekelezaji unakuwa haupo.
“Hivi sasa tuna daftari mtu akija kushtakiwa anatakiwa alete
hela hapa ofisini na huyo mwanamke
aifuate hapo. Mwanamme anapopeleka hela anasaini na mwanamke anapochukua pia,”
anasema na kuongeza kuwa kesi hizo zinazidi 30.
JINSI YA KUPANGILIA MALENGO YAKO NA LUCY NGOWI
JINSI YA KUPANGILIA MALENGO YAKO
SOMAJI wangu, nakukaribisha tena katika mfululizo wa makala
hizi za maisha yetu, zinzokujia kila Alhamisi.
Leo tutaangalia jinsi unavyoweza kupanga malengo makubwa katika maisha yako.
Watu wengi hushindwa kufikia malengo makubwa kwa kuwa, mara zote hujikatisha tamaa kuwa hawawezi kufanya jambo kubwa la kimaendeleo, kabla ya kujaribu kulifanya.
Tabia ya baadhi ya watu hao wanaokuwa na malengo madogo katika mazingira wanayoishi, ina maanisha eneo hilo hakuna ushindani wa kimaendeleo, ama wao wenyewe hawana jitihada za dhati za kupiga hatua zaidi mbele.
Lakini ikimbukwe kuwa, katika kutafuta mafanikio hayo ili uwe na maisha bora, usimwangalie mtu jinsi alivyo, kwamba ana urefu gani, ana pesa kiasi gani, digrii aliyonayo ama kuangalia historia ya maisha yake, bali hupimwa kwa uwezo wa kufikiri kwake.
Watu wengi wanaofikiria kuwa na malengo makubwa ya mafanikio, katika maisha yao ni kutokana na matarajio waliyonayo.
Inakupasa kila mara ujitahidi kupanua mawazo yako na kubuni mbinu mpya za kukutoa hapo ulipo na kukuweka katika hatua nyingine nzuri zaidi kimaendeleo.
Hivyo utambue kuwa, unapotaka kufanya mambo makubwa inakupasa ujijue wewe ni nani na una thamani gani.
Kwa maelezo mengine usijishushe hadhi yako kwa kuona kuwa huwezi kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo ambayo yatakutoa hapo ulipo na kukuweka katika hatua nyingine nzuri zaidi.
Tuangalie mfano wa kijana mmoja aliyeshindwa kupiga hatua mbele baada ya kujishusha hadhi yake na kujiona hawezi.
Kijana huyo, aliona tangazo la kazi katika gazeti. Kazi aliyokuwa anapenda kuifanya na pia ameisomea.
Lakini hakufanya jitihada za dhati za kuomba nafasi ile, kwa kuwa alijiona hawezi kuipata hata kama angeomba.
Aliona kuliko ajitaabishe ni heri aache kuomba nafasi hiyo. Mfano huo si mzuri kwa mtu anayetaka kupiga hatua kimaisha.
Usijishushe hadhi yako ama usikatishwe tamaa kwa hali yoyote ile. Ni vema kujaribu kile unachokipenda na unachokihitaji katika maisha yako, kuliko kuacha kujaribu kwa kuogopa kuwa hautafanikiwa.
Kwani matokeo huja baadaye, hata utakaposhindwa, utakuwa na nguvu ya kujaribu tena sehemu nyingine.
Wengi wetu, tumekuwa tukijikatisha tamaa katika shughuli mbalimbali tuzifanyazo ama tunazotaka kuzifanya.
Yawezekana umeanzisha biashara kwa lengo la kukuinua kiuchumi, lakini matokeo yake, biashara hiyo haiendi kama vile ulivyotarajia.
Jambo la msingi, inakupasa kukaa chini na kujitathmini, kuangalia ni sehemu gani unayokosea.
Ama kuangalia, kama una washindani wengi katika eneo hilo, ili uweze kufanya vizuri zaidi yao, kwa kuweka vitu vingi tofauti na kuboresha eneo la biashara yako.
Kuwa mbunifu katika biashara yako kutakupa wateja wengi, na utafanikiwa zaidi. Cha msingi usikate tamaa katika kufikia malengo unayoyakusudia.
Kutokana na hali ya kujikatisha tamaa, miongoni mwa watu wengi, wanasaikolojia mbalimbali wamekuwa wakishauri ni vema, watu wajijue vile walivyo ili waweze kujirekebisha pale penye upungufu na kusonga mbele kimaisha.
Hali ya kujikatisha tamaa ni mbaya sana, ni sawa na ugonjwa usiopona katika mwili wako. Ili kuutibu ugonjwa huo, inakupasa ujielewe wewe ni nani, na una upungufu gani, pamoja na kukubali mabadiliko.
Tatizo kubwa lililopo kwa watu wengi, hawajui kuwa, wao wana uwezo mkubwa tofauti na wanavyojifikiria.
Hivyo ni vema kuweka mawazo yako kwenye kipimo halisi, uyachuje na kuchukua yale yaliyo na thamani.
Penda kufikiri mambo makubwa. Usijishushe hadhi yako kwa kujiwekea au kufikiri malengo madogo. Anza sasa kuwaza mambo makubwa ili uwe mtu mwenye ndoto njema ya maendeleo.
Kutokana na hali hiyo ya watu kujikatisha tamaa, wale ambao wamewahi kufanya biashara na kufilisika, wengi wao wamekuwa wakisema kuwa hawatarudia tena kufanya biashara hiyo.
Lakini kumbe, haikuwapasa kukata tamaa, bali kujipa moyo, na kuelewa kuwa pamoja na hali hiyo ya kushindwa inawapasa kujaribu tena.
Kamwe usikate tamaa katika jambo lolote unaloliwaza ama kulifanya. Kwa kuwa, upo msemo mmoja unaosema, penye nia pana njia.
Tukutane wiki ijayo.
Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa kitabu cha ‘The Magic of Thinking Big’, kilichotungwa na David Schwartz pamoja na mitandao mbalimbali.
Leo tutaangalia jinsi unavyoweza kupanga malengo makubwa katika maisha yako.
Watu wengi hushindwa kufikia malengo makubwa kwa kuwa, mara zote hujikatisha tamaa kuwa hawawezi kufanya jambo kubwa la kimaendeleo, kabla ya kujaribu kulifanya.
Tabia ya baadhi ya watu hao wanaokuwa na malengo madogo katika mazingira wanayoishi, ina maanisha eneo hilo hakuna ushindani wa kimaendeleo, ama wao wenyewe hawana jitihada za dhati za kupiga hatua zaidi mbele.
Lakini ikimbukwe kuwa, katika kutafuta mafanikio hayo ili uwe na maisha bora, usimwangalie mtu jinsi alivyo, kwamba ana urefu gani, ana pesa kiasi gani, digrii aliyonayo ama kuangalia historia ya maisha yake, bali hupimwa kwa uwezo wa kufikiri kwake.
Watu wengi wanaofikiria kuwa na malengo makubwa ya mafanikio, katika maisha yao ni kutokana na matarajio waliyonayo.
Inakupasa kila mara ujitahidi kupanua mawazo yako na kubuni mbinu mpya za kukutoa hapo ulipo na kukuweka katika hatua nyingine nzuri zaidi kimaendeleo.
Hivyo utambue kuwa, unapotaka kufanya mambo makubwa inakupasa ujijue wewe ni nani na una thamani gani.
Kwa maelezo mengine usijishushe hadhi yako kwa kuona kuwa huwezi kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo ambayo yatakutoa hapo ulipo na kukuweka katika hatua nyingine nzuri zaidi.
Tuangalie mfano wa kijana mmoja aliyeshindwa kupiga hatua mbele baada ya kujishusha hadhi yake na kujiona hawezi.
Kijana huyo, aliona tangazo la kazi katika gazeti. Kazi aliyokuwa anapenda kuifanya na pia ameisomea.
Lakini hakufanya jitihada za dhati za kuomba nafasi ile, kwa kuwa alijiona hawezi kuipata hata kama angeomba.
Aliona kuliko ajitaabishe ni heri aache kuomba nafasi hiyo. Mfano huo si mzuri kwa mtu anayetaka kupiga hatua kimaisha.
Usijishushe hadhi yako ama usikatishwe tamaa kwa hali yoyote ile. Ni vema kujaribu kile unachokipenda na unachokihitaji katika maisha yako, kuliko kuacha kujaribu kwa kuogopa kuwa hautafanikiwa.
Kwani matokeo huja baadaye, hata utakaposhindwa, utakuwa na nguvu ya kujaribu tena sehemu nyingine.
Wengi wetu, tumekuwa tukijikatisha tamaa katika shughuli mbalimbali tuzifanyazo ama tunazotaka kuzifanya.
Yawezekana umeanzisha biashara kwa lengo la kukuinua kiuchumi, lakini matokeo yake, biashara hiyo haiendi kama vile ulivyotarajia.
Jambo la msingi, inakupasa kukaa chini na kujitathmini, kuangalia ni sehemu gani unayokosea.
Ama kuangalia, kama una washindani wengi katika eneo hilo, ili uweze kufanya vizuri zaidi yao, kwa kuweka vitu vingi tofauti na kuboresha eneo la biashara yako.
Kuwa mbunifu katika biashara yako kutakupa wateja wengi, na utafanikiwa zaidi. Cha msingi usikate tamaa katika kufikia malengo unayoyakusudia.
Kutokana na hali ya kujikatisha tamaa, miongoni mwa watu wengi, wanasaikolojia mbalimbali wamekuwa wakishauri ni vema, watu wajijue vile walivyo ili waweze kujirekebisha pale penye upungufu na kusonga mbele kimaisha.
Hali ya kujikatisha tamaa ni mbaya sana, ni sawa na ugonjwa usiopona katika mwili wako. Ili kuutibu ugonjwa huo, inakupasa ujielewe wewe ni nani, na una upungufu gani, pamoja na kukubali mabadiliko.
Tatizo kubwa lililopo kwa watu wengi, hawajui kuwa, wao wana uwezo mkubwa tofauti na wanavyojifikiria.
Hivyo ni vema kuweka mawazo yako kwenye kipimo halisi, uyachuje na kuchukua yale yaliyo na thamani.
Penda kufikiri mambo makubwa. Usijishushe hadhi yako kwa kujiwekea au kufikiri malengo madogo. Anza sasa kuwaza mambo makubwa ili uwe mtu mwenye ndoto njema ya maendeleo.
Kutokana na hali hiyo ya watu kujikatisha tamaa, wale ambao wamewahi kufanya biashara na kufilisika, wengi wao wamekuwa wakisema kuwa hawatarudia tena kufanya biashara hiyo.
Lakini kumbe, haikuwapasa kukata tamaa, bali kujipa moyo, na kuelewa kuwa pamoja na hali hiyo ya kushindwa inawapasa kujaribu tena.
Kamwe usikate tamaa katika jambo lolote unaloliwaza ama kulifanya. Kwa kuwa, upo msemo mmoja unaosema, penye nia pana njia.
Tukutane wiki ijayo.
Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa kitabu cha ‘The Magic of Thinking Big’, kilichotungwa na David Schwartz pamoja na mitandao mbalimbali.
Kwa maoni, ushauri wasiliana nasi nami kwa
simu 0713 331455; 0767331455
FAHAMU KANUNU ZA KUISHI VIZURI na LUCY NGOWI lucyngowi2009@gmail.com
FAHAMU KANUNU ZA KUISHI VIZURI
na LUCY NGOWI
lucyngowi2009@gmail.com
KARIBUNI tena wapenzi wasomaji wa safu hii ya kila Alhamisi.
Wiki iliyopita tulizungumzia kuhusu kuepuka tabia ya ukali, ukaidi na ugomvi.
Leo tutaona kanuni au mbinu nyingine za kuishi na watu vizuri, ukiwa ni
mwendelezo wa pale ilipoishia.
Epukana na biashara au na shughuli zisizo halali. Unapofanya shughuli au biashara isiyo halali inakuondolea uaminifu kwa jamii inayokuzunguka.
Kwa mfano, kama mtaani au kazini kwako unakuwa mtu usiyeeleweka kwa kuwa watu wanajiulizauliza kile unachofanya na wasipate majibu, hiyo si jinsi au njia nzuri ya kuishi na watu.
Vile vile biashara hizo zinaweza kukusababishia matatizo kama ya kufunguliwa mashitaka na kufikishwa mahakamani endapo utakutwa na kosa.
Jifunze kutokuwa mchoyo au uwatakie watu wengine mambo mema. Baadhi ya watu waliofanikiwa huwa hawapendi maendeleo ya wengine. Wanapoombwa msaada ni wagumu kutoa.
Mfano kwa baadhi ya wanafunzi shuleni wakiojaaliwa kuwa na uwezo kiakili huwa hawapendi kutoa msaada kwa wenzao. Hata maofisini kuna baadhi ya watu wasiopendi maendeleo ya wenzao kwa kumsemea mambo yasiyo ya kweli kwa bosi wao.
Epukana na lugha ya ubinafsi, mfano: mimi, changu, n.k. Badala yake tumia chetu, sisi n.k. Lugha hizo si nzuri katikati ya jamii inayokuzunguka. Unapokuwa na tabia hiyo inakujengea chuki miongoni mwa wanaokuzunguka. Ni vizuri kushirikiana vifaa vya ofisini, shuleni na katika maeneo mbalimbali na jamii.
Inawezekana wakati mwingine mtu anakuwa na lugha hiyo ya ubinafsi kutokana na mazingira yaliyopo. Mfano wewe ni msafi na wenzake unaoishi nao, kufanya kazi nao au kusoma nao wanakuwa na tabia ya uchafu. Kama umeshajaribu kuwabadilisha bila mafanikio, ni vizuri kutumia busara ya kununua vitu kama vyako na kuwapa vile ambavyo una uwezo navyo.
Hii itakusaidia kila mtu kutumia kifaa chake, mfano vikombe maofisini - kila mtu ana usafi wake, vioo kwa akina dada, chanuo za kuchania nywele na mfano wa vitu kama hivyo. Jitahidi kutokuonyesha hali hiyo kwa gharama yoyote ile.
Thamini utu wa mtu bila kujali uwezo au nafasi yake katika jamii. Kumbuka kwamba siku hazifanani, kwani waweza kupokea msaada mkubwa wa kimawazo au wa hali kutoka kwa mtu usiyemtarajia.
Watu wengine wanapotoa msaada kwa wenzao hujisahau na kuanza kutangaza au kumnyanyapaa yule aliyemsaidia huku akiona ni sawa.
Mfano rahisi unakuta labda kuna watu wengine wamewapokea ndugu zao au watu ambao hawana uwezo na kuishi nao nyumbani kwao. Kutokana na kuishi naye basi ufadhili unageuka kuwa mateso kwa kuwa kila kazi ataifanya huyo aliyesaidiwa au kila mara atakuwa anatumwa maeneo ya mbali mara nyingine pasipo hata na nauli.
Si vibaya kumtuma wala si vibaya kusaidiwa na mtu kama huyo, ila isivuke mipaka kwani itakujengea picha mbaya kwa wanaokufahamu pamoja na huyo unayemsaidia atakapoamua kuondoka kwako.
Epukana na tabia ya kugombeza, kutukana au kudharau wengine. Iwapo watu walio chini yako wamekosea au wamefanya kinyume na ulivyotarajia; jaribu kuwaelekeza kwa upole bila kutumia jazba au hasira. Usiendekeze lugha za matusi, dharau au ugomvi, kwani huweza kushusha hadhi yako na hata utu wako.
Watu wengine wamejiendekeza katika tabia ya kupenda kugombagomba ovyo hata bila sababu, wengine hudiriki hata kutukana au kudharau wengine.
Hii ipo sana maofisini. Mabosi walio wengi hujisahau kuwa nafasi wanazokalia ni za muda tu, hivyo hudharau wale walio chini yao kwa kuwasemasema ovyo na kuwatukana pasipo sababu ya msingi.
Hata kwa upande wa baadhi ya wanawake na wanaume wawapo nyumbani kwao huwa na tabia hiyo kwa watoto wao, wafanyakazi waliowaajiri au ndugu wanaoishi nao.
Ni vizuri kuacha tabia hiyo, kwani inakuondolea heshima na kukufanya udharaulike.
Pia wakati mwingine utakuta wenye mali si wasemaji, lakini wale wanaowaachia majukumu kidogo ndiyo wanaokuwa na tabia hizo mbaya katika jamii. Gombeza pale inapostahili lakini isiwe mazoea, kamwe usitukane wala kuleta dharau kwa wengine. Huo ni utovu wa nidhamu.
Jifunze kuvumilia mienendo ya imani ya dini nyingine. Watu wengine wana tabia ya kudharau au kutothamini misimamo ya wengine ya kiimani. Utamkuta mtu anakashifu hadharani dini za watu wengine kwa kutumia vigezo visivyokuwa na maana.
Suala hili katika jamii yetu inayotuzunguka limekuwa likileta mizozano na wakati mwingine watu huamua kupigana. Mnapokuwa watu wenye imani za dini tofauti katika ofisi zenu, vyuoni au hata kwenye mikusanyiko mbalimbali, jaribu kuvumilia kila hatua ambayo kwako unaiona ni kinyume na maadili yako. Ukishindwa hali hiyo ni vizuri uondoke na kuwapisha wenyewe waendelee.
Kwa mfano, kwenye msiba labda wewe ni wa madhehebu fulani, hivyo umekwenda kwenye msiba wa imani tofauti na yako, ni vizuri kufuata taratibu zilizopo mahali pale, na kama unajiona huwezi basi ili kuepusha shari ondoka eneo hilo uwaachie wenyewe ili usionekane ni kituko.
Ni vizuri ukae kimya uwaachie wenyewe waendelee na ratiba na shughuli zao kuliko kuanza kupayuka ovyo au kukosoa katika msiba huo. Tulia wakimaliza shiriki nao kwenye msiba ndivyo maisha yalivyo.
Usiwe mkali kwa watu, jenga uhusiano mzuri. Ukali ni hulka ambayo huwafanya watu wawe mbali na wewe na hata kusababisha kukosa marafiki. Unaweza kukuta mtu ana nafasi nzuri katika jamii lakini hakuna mtu mwenye mazoea naye kutokana na ukali wake. Mfano katika ofisi mwajiri unakuwa mkali kiasi kwamba wafanyakazi wako wanakosa uhuru wa kujieleza kwako wanapokuwa na matatizo yao binafsi au ya kiofisi.
Unapokuwa na uhusiano mzuri na watu; hali hiyo inakufanya kukubalika, kuheshimika, kupendwa na jamii inayokuzunguka. Mfano mwalimu anapokuwa karibu na wanafunzi wake, huweza kuvuta hisia zao za usikivu na hatimaye kufanya vema katika masomo yao.
Uwe mwangalifu sana na mwanamke/mwanaume asiyekuwa wako. Siku zote mazoea na watu wa jinsia tofauti na ya kwako lazima yawe na mipaka. Kuna watu ambao hawawezi kutawala hisia zao hata wanapokuwa na wenzao ambao tayari wana familia zao.
Hii inajitokeza sana shuleni, vyuoni, maofisini na hata maeneo ya kuishi; unakokuta msichana au kijana anakuwa na mazoea yaliyopitiliza na mume au mke wa mtu, hali inayoweza kusababisha mtafaruku kati ya pande husika.
Wakati mwingine unakuta wanawake/wanaume waliooa au kuolewa wanakuwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa zao, hali inayosababisha kutoelewana baina yao na wenzi wao; wakati mwingine hata kusababisha kuvunja ndoa zao.
Kwa maoni, ushauri wasiliana nasi nami kwa
simu 0713 331455; 0767331455
ACHA MAWAZO FINYU
KATIKA makala zangu za Maisha Yetu niliwahi kuandika kwamba
njia pekee ya kufanikiwa ni kutoruhusu mawazo yanayoleta kizuizi, kama vile kuwaza umaskini, kuwa na hofu au wasiwasi kila
mara kwa kile unachokifanya.
Endapo wewe ni mtu wa aina hiyo inakupasa ubadilike ili usonge mbele kimafanikio.
Mara tu unapomaliza kuyachuja mawazo yako, unachagua yale unayotaka kuyafanyia kazi. Utagundua kuwa nayo yanahitaji kuongezewa ubora wake. Jifunze kutokufunga milango yako ya kuwa mbunifu.
Endapo wewe ni mtu wa aina hiyo inakupasa ubadilike ili usonge mbele kimafanikio.
Mara tu unapomaliza kuyachuja mawazo yako, unachagua yale unayotaka kuyafanyia kazi. Utagundua kuwa nayo yanahitaji kuongezewa ubora wake. Jifunze kutokufunga milango yako ya kuwa mbunifu.
Ni jambo lisilowezekana kati yetu kuwa kinyume cha ujuzi tulionao.
Mfano mtu hawezi kupita mbele ya gari liendalo kasi kwa kuwa anajua kuwa ataumia, hawezi kuogelea baharini kama anajua atazama, hawezi kuwa mstari wa mbele katika jambo la hatari kama anajua kuwa atadhurika.
Mafanikio hayahitaji kuwa na kiasi kikubwa cha ujuzi juu ya jambo fulani, lakini unatakiwa kung’ang’ania ili uweze kupata mafanikio hayo kwa ujuzi wowote ulionao.
Mkulima mmoja aliyejulikana kwa jina la Walter na ambaye siku za usoni angependa kuwa mchezaji bora wa mpira wa miguu, alimuuliza rafiki yake kuwa amewezaje kupata sh milioni 10 katika kazi yake anayoifanya kutokana na ujuzi alionao na kuweza kushinda kila dhana ya kushindwa ambayo ilikuwa inaibuka katika utendaji wake?
Rafiki huyo alimjibu kuwa wakati anaanza, alijua anataka kufanya nini na anachotarajia kukipata.
Alikuwa na njozi iliyomwezesha kujenga picha katika mawazo yake kulingana na malengo aliyotaka kuyafikia katika maisha yake.
Hivyo hiyo ndiyo siri kubwa ya mafanikio katika maisha yake.
Walter anasema kuna wakati alisikia umati wa watu ukishangilia katika mawazo yake.
Kuna wakati alijenga picha ya sherehe ya kupewa tuzo iliyojaa waandishi wa habari za michezo, wageni na wanamitindo mbalimbali.
Ndoto hiyo sasa ameanza kuifanyia kazi, hivyo anaamini atafanikiwa kama rafiki yake huyo alivyofanikiwa.
Inaonesha watu wengi wamekuwa hawako tayari kutulia na kufanyia kazi ndoto zile wanazokuwa nazo, kwa kuzipa nafasi ndogo katika utekelezaji wake.
Kuna mamilioni ya watu wanaoamini wanaangamia kwa umaskini na kushindwa kwa sababu baadhi ya malengo waliyonayo wamekuwa hawawezi kuyafanyia kazi.
Bila kujua watu wengi hujitengenezea mazingira mabaya kutokana na mawazo hasi yanayochukuliwa na mawazo na kutafsiriwa kwenda katika vitendo.
Kwa sasa hivi utaweza kutambua kwamba mawazo ni vitu ambavyo kama vikifanyiwa kazi vizuri na kutekelezwa vinaweza kuwekwa katika mfumo wa uhalisia.
Kama utakuwa na njozi za kupata zaidi na ukazijengea picha hiyo bila kujali utakumbana na vikwazo gani, hiyo itakuwa ni vipaumbele katika maisha yako.
Kama utaruhusu picha ya namna hii kuwa ya kudumu katika ulimwengu wako wa mawazo; utafikiri mawazo ya mafanikio na kuzungukwa na watu wenye mafanikio watakaotia moyo njozi zako.
Utatenga sehemu ya kipato chako kwa ajili ya kujilipa wewe mwenyewe, moja ya hatua muhimu katika kupata utajiri.
Utajihusisha katika mpango unaoleta mafanikio binafsi na kukufanya uchague lengo la maisha yako.
Pia utatafuta ujuzi na utaalamu kwa wale wote ambao wamefanikiwa. Mwishoni utafanikiwa licha ya kukumbana na vikwazo katika kutekeleza njozi zako.
Kwa maoni, ushauri wasiliana nasi nami kwa
simu 0713 331455; 0767331455
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)